![]() |
Yukio Amano |
Yukio Amano, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA anatarajiwa kuwasili hapa nchini Iran Jumapili, Mei 20 kwa ziara rasmi ya siku moja. Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ali Akbar Salehi amesema kuwa ziara ya Bw. Amano ni katika kalibu ya mazungumzo mapya yenye lengo la kuondoa suitafahumu iliyoko kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran na kwamba inatarajiwa muafaka wa pamoja utafikiwa.
Amano anatarajiwa kuandamana na naibu wake anayehusika na masuala ya sera Rafael Grossi pamoja na mkuu wa timu ya waangalizi wa IAEA, Herman Nackaerts kwenye safari yake hiyo.
Mazungumzo ya mwisho yaliyofanyika kati ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki yalikuwa yale ya wiki jana Mei 14 mjini Vienna na wachambuzi wa mambo wanaitakidi kuwa safari ya Yukio Amano hapa Tehran inaweza kusaidia kutatua baadhi ya mambo katika ushirikiano wa pande mbili.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kuwa na tatizo la kujenga uaminifu kati yake na IAEA na mara zote imekuwa ikijibu maswali yote ya wakala huo kuhusiana na miradi yake ya nyuklia yenye malengo ya amani. Mbali na kusisitiza kuwa miradi yake ya nyuklia ni ya amani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza utayarifu wake wa kushirikiana na wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA na kwa msingi huo pia IAEA inafaa kuondoa tuhuma zake zisizo na msingi dhidi ya Iran na vilevile kukomesha mashinikizo yake ya kisiasa dhidi ya Tehran.Amano anatarajiwa kuandamana na naibu wake anayehusika na masuala ya sera Rafael Grossi pamoja na mkuu wa timu ya waangalizi wa IAEA, Herman Nackaerts kwenye safari yake hiyo.
Mazungumzo ya mwisho yaliyofanyika kati ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki yalikuwa yale ya wiki jana Mei 14 mjini Vienna na wachambuzi wa mambo wanaitakidi kuwa safari ya Yukio Amano hapa Tehran inaweza kusaidia kutatua baadhi ya mambo katika ushirikiano wa pande mbili.
Weledi wa mambo wanasema kuwa, kutengenezwa faili bandia dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran ni matunda ya mashinikizo ya Marekani na utendakazi usio wa wazi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki. Hii ni katika hali ambayo mwaka 2007 Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikubaliana na IAEA kuhusu njia za kuondoa hali ya kutoaminiana na katika makubaliano hayo Iran ikajibu maswali sita yaliyokuwa na utata na hivyo IAEA kupitia mkurugenzi wake mkuu wa wakati huo Mohamed El- Baradei ikasema majibu ya Iran yalikuwa ya kuridhisha na hivyo kufunga mjadala huo. Mbali na hayo, wakaguzi wa IAEA wamekuwa wakitembelea taasisi za nyuklia za Iran na hawajawahi kutoa ripoti yoyote inayoonyesha kuwa miradi ya nyuklia ya Iran imekengeuka mkondo wa amani. Lakini pamoja na hayo, ukiwa chini ya mashinikizo ya kisiasa kutoka nchi za Magharibi, wakala wa IAEA umeshindwa kulirudisha katika hali ya kawaida faili la nyuklia la Iran na hivyo kuendelea kubakia katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Licha ya vikwazo hivyo vyote, Iran imekuwa ikiyapa umuhimu mazungumzo yake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki. Kwa msingi huo weledi wa mambo wanasema kuwa huenda safari hii ya Yukio Amano hapa Tehran ikiwa ni fursa nzuri kwa wakala wa IAEA kuithibishia serikali ya Tehran kwamba uko tayari kubadilisha siasa zake za huko nyuma na kushirikiana vizuri na kwa uaminifu na viongozi wa Tehran kuhusiana na mpango wake wa nyuklia.
No comments:
Post a Comment