Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, May 26, 2012

Mwanasiasa mmoja auawa huko kaskazini mashariki mwa Nigeria

Watu wasiojulikana wenye silaha wamemuua mkuu wa chama cha Ukweli kwa Wananchi huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Polisi ya nchi hiyo imetangaza kuwa Alhaj Ahmadu mkuu wa chama cha Ukweli kwa Wananchi ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika mji wa Gombe nchini humo. Viongozi wa ngazi za juu wa eneo hilo nchini Nigeria wametangaza kuwa, kundi lenye misimamo ya kufurutu ada la Boko Haram lina mkono katika tukio hilo. Aidha polisi nchini humo tayari wameanza uchunguzi wa mauaji hayo. Kufuatia habari hiyo vikosi vya Nigeria vimeanzisha oparesheni kali ya kuzikagua nyumba zinazosadikiwa kumilikiwa na wafuasi wa kundi la Boko Haram.

No comments: