Jabeur Mejri (Kulia) na Ghazi Beji, Watunisia waliomvujia heshima Mtume Muhammad SAW
Kesi ya mtu aliyemvunjia heshima Mtume Mtukufu Muhammad SAW inatarajiwa kuendelea kusikilizwa siku ya Jumatatu nchini Tunisia.
Habari zinasema kuwa, siku ya Jumatatu Mahakama ya Rufaa nchini Tunisia itasikiliza rufaa iliyokatwa na Jabur Majra aliyehukumiwa kwenda jela miaka saba na nusu jela kufuatia kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Itakumbukwa kuwa tarehe 28 mwezi Machi mwaka huu, mahakama moja nchini Tunisia iliwahukumu kifungo cha miaka saba na nusu wanafunzi wawili kwa tuhuma za kusambaza picha chafu zinazomvunjia heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu SAW. Wanafunzi hao wanajulikana kwa majina ya Jabru Majra na Ghazi Biji.
Wakati huo huo maandamano makubwa ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu yaliyofanyika nchini humo hii leo kulalamikia ukosefu wa ajira na hali nguvu ya maisha yamevunjwa na vikosi vya Tunisia katika mji wa Kifu.

No comments:
Post a Comment