
Kikosi cha AMISON kikishirikiana na serikali ya Somalia kimeshadidisha mapigano dhidi ya ngome ya waasi hao katika mji wa Afgooye ulioko magharibi mwa mji mkuu Mogadishu na kuudhibiti mji huo.
Suala hilo limepelekea mamia ya wananchi wa Somalia kukimbia nyumba zao na kuelekea katikati mwa mji mkuu Mogadishu. Kikosi cha AMISON kikishirikiana na wanajeshi wa Somalia kilianza mashambulio hayo katika mji wa Daniel pambizoni mwa mji mkuu Somalia. Mapigano hayo yaliyojiri jana yamepelekea watu wasiopungua 16 kuuawa.
No comments:
Post a Comment