Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 23, 2012

Pendekezo la Iran kwa kundi la 5+1 katika mazungumzo ya Baghdad

Iran imewasilisha kifurushi cha mapendekezo kamili kwa wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani (5+1).
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mehr, Saeed Jalili mwakilishi mkuu wa Iran katika mazungmzo ya nyuklia aliwasilisha pendekezo hilo Jumatano ya leo katika awamu ya kwanza ya mazungumzo ya Iran na kundi la 5+1 mjini Baghdad. Duru zimedokeza kuwa kifurushi hicho cha mapendekezo kamili kinajumuisha nukta tano zikiwemo kuhusu masuala ya nyuklia na yasiyo ya nyuklia. Duru zilizokaribu na timu ya mazungumzo ya Iran zimearifu kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijalegeza misimamo yake ya kimsingi. Mazungumzo ya Baghdad yanatazamiwa kuendelea Alkhamisi. Mapema leo Michael Mann msemaji wa Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amesema umoja huo unatambua haki ya Iran ya kunufaika na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani.

No comments: