Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 23, 2012

'Vijana wa Iran watauletea fakhari umma wa Kiislamu'

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema Wairani wana matumaini kuhusu mustakabali na kuongeza kuwa, nchi hii ni ya vijana ambao wanapaswa kulielekeza taifa hili la Kiislamu katika adhama na hatimaye kuweza kuuletea fakhari na mafanikio makubwa umma wote wa Kiislamu.
Akizungumza katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Maafisa wa Kijeshi cha Imam Hussein AS mjini Tehran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema adhama na hadhi inayozidi kuimarika ya taifa la Iran inatokana na mapambano na istikama ya vijana wa Iran katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Kiongozi Muadhamu ameendelea kusema kuwa, taifa lililoko mstari wa mbele la Iran, litaongeza kasi yake ya kujiletea maendeleo makubwa zaidi na kusimamisha uadilifu sambamba na kupambana vilivyo na kambi ya dhulma, mabeberu na waistikbari katika muongo huu wa maendeleo na uadilifu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Amesema, licha ya kwamba madola ya kibeberu yanajionesha kwa walimwengu kuwa yana nguvu, lakini ukweli ni kwamba madola hayo yanazidi kudhoofika na nguvu zao zinazidi kudidimia kadiri siku zinavyosonga mbele. Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amepongeza mapambano ya vikosi vyote vya kijeshi vya Iran katika vita vya kulazimishwa vya Iraq vya miaka minane katika muongo wa thamanini. Amesema uzoefu katika miaka hiyo unapaswa kuwa nuru ya kuliongoza taifa katika mustakabali.
Mahafali hiyo pia ilifanyika sambamba na siku ya kwanza ya Mwezi wa Rajab na kumbukumbu ya Siku ya Kuzaliwa Imam Muhammad Baqir AS mmoja wa wajukuu watukufu wa Mtume Muhammad SAW. Mahafali hiyo aidha imesadifiana na siku ya kukumbuka ukombozi wa mji wa Iran wa Khorramshar uliokuwa umekaliwa kwa mabavu na jeshi la Iraq mwaka wa 1983.

No comments: