Mahakama ya kijeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetoa hukumu mbalimbali kwa takriban wanajeshi 13 walioasi jeshini miezi miwili iliyopita. Makamanda 2 ambao hawakuwa mahakamani wamehukumiwa kifo huku wanajeshi wengine 8 waliokuwa mahakamani wakihukumiwa vifungo vya maisha. Wanajeshi 3 walipewa vifungo vya kati ya miaka 2 na 200 jela. Mahakama hiyo ya kijeshi katika mji wa Bukavu imesema kuwa hatua ya wanajeshi kuasi ilichukuliwa katika mkutano uliofanyika mwezi Machi mjini Goma na kuhudhuriwa na Jenerali Bosco Ntaganda ambaye kwa sasa anasakwa na majeshi ya serikali. Mapigano mapya kati ya wanajeshi walioasi na wale wa serikali mashariki mwa nchi hiyo yamepelekea makumi ya maelfu ya raia kukimbia makaazi yao na kutafuta hifadhi katika nchi jirani za Rwanda na Uganda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment