Bunge la Uganda limefanya uchaguzi wa wawakilishi wa nchi hiyo katika baraza la Afrika Mashariki. Hatua hiyo imekamilisha shughuli za nchi tano za kuwachagua wawakilishi wao katika bunge hilo la kiukanda. Uchaguzi huo ulijaa joto la ushabiki kwa wagombezi wote 17 waliojitokeza kuwania nyadhifa tisa zilizokuwa zinahitajika huku kila mgombezi akipewa fursa maalumu ya kujielezea katika kampeni za kujivutia kura katika uchaguzi huo. Wagombezi hao walitoka chama tawala, vyama vya upinzani pamoja na vile vinavyojitegemea. Waliofaulu kuingia katika bunge la Afrika Mashariki ni pamoja na Byamukama Dora, Ssebalu Mike, Zziwa Margaret, Tiperu Nusura, Kidega Daniel, Mukasa Fred Mbidde, Mulengani Bernard, Opoka Okumu na Nakawuki Suzan. Matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa na Spika wa Bunge la taifa Rebecca Kadaga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment