Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, May 24, 2012

Alkhamisi, Mei 24, 2012


Leo ni Alkhamisi tarehe Pili Rajab mwaka 1433 Hijria inayosadifiana na tarehe 24 Mei mwaka 2012 Miladia.Siku kama ya leo miaka 12 iliyopita, vikosi vya utawala dhalimu wa Israel vililazimika kuondoka kwa madhila katika eneo la kusini mwa Lebanon baada ya kulikalia kwa mabavu eneo hilo kwa muda wa miaka 22. Majeshi hayo yaliondoka baada ya kushindwa kukabiliana na mapambano ya wananchi wa kusini mwa Lebanon. Ilikuwa mwaka 1978, wakati jeshi la Israel lilipoishambulia Lebanon kwa mara ya nne. Mwaka 1982, majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yalianza tena kuishambulia Lebanon na kusonga mbele hadi katika mji mkuu wa nchi hiyo Beirut. Hata hivyo kutokana na wananchi hao kuathirika na mafunzo ya kutokubali dhulma hasa baada ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, nchini Lebanon kulianzishwa harakati za mapambano ya Kiislamu dhidi ya majeshi vamizi ya utawala haramu wa Israel.
Chama cha Hizbullah kilikuwa na nafasi muhimu na ya kuzingatiwa mno katika kukombolewa eneo la kusini mwa Lebanon toka katika makucha ya utawala dhalimu wa Israel. ***
Miaka 19 iliyopita na katika siku kama ya leo, nchi ya Eritrea iliyoko kaskazini mashariki mwa bara la Afrika ilipata uhuru kutoka kwa Ethiopia. Mwaka 1936 Italia iliikalia kwa mabavu Eritrea iliyokuwa ikihesabiwa katika zama hizo kuwa ni sehemu ya ardhi ya Ethiopia. Mwaka 1953, Italia iliirejeshea Ethiopia ardhi hiyo. Hata hivyo wananchi wengi wa nchi hiyo waliokuwa wakitaka uhuru walianzisha harakati za ukombozi dhidi ya serikali ya Ethiopia. Mwaka 1991, Harakati ya Ukombozi wa Eritrea ikisaidiana na wanamapinduzi wa Ethiopia walihitimisha utawala wa kidikteta wa Mengistu Haile Mariam, na wakakubaliana kuanishwa mustakbali wa Eritrea mwaka 1993 kwa kura ya maoni. Washiriki wengi wa kura hiyo ya maoni walipiga kura ya kutaka kujitawala Eritrea. ***
Na siku kama ya leo miaka 993 iliyopita, aliaga dunia Abu Rayhan Biruni msomi stadi na mahiri wa Kiirani. Tangu anaanza kusoma, Abu Rayhan Biruni alikuwa na mapenzi makubwa na maalumu na elimu ya hisabati. Hima na bidii yake ilifanya muda si mrefu ajitokeze na kuwa mwalimu mkubwa katika elimu ya hisabati.

No comments: