Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan amesema kuwa, mkono wa Israel unaonekana waziwazi katika shambulizi kali la kigaidi lililoharibu vibaya gari moja na kumuua mfanyabiashara mmoja huko Port Sudan.
Bw. Ali Ahmed Karti ameiambia televisheni ya ash Shoroug kwamba, dalili zote zinaonesha kuwa shambulio hilo limeendeshwa kwa msaada wa Israel kwani linafanana kabisa na mashambulizi mengine kama hayo yaliyowahi kushuhudiwa kwenye maeneo mengine ya jimbo hilo la Bahari Nyekundu.
Amesema, utawala wa Kizayuni wa Israel unadhani kuwa, Sudan inayaunga mkono makundi na vyama vya Kipalestina vinavyopinga utawala wa Kizayuni.
Itakumbukwa kuwa juzi Jumanne, shambulio moja la kigaidi lililenga gari ya mfanyabishara Nasir Awadh Ahmad Saeed katika mji wa Port Sudan wa jimbo la Bahari Nyekundu saa mbili asubuhi kwa saa za huko na kumuua papo hapo mfanyabiashara huyo.

No comments:
Post a Comment