Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, May 24, 2012

Kijana kizimbani kwa kulawiti watoto

MKAZI wa Vingunguti kwa Simba Selemani Thabit (18) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili ya kulawiti watoto mwenye umri wa miaka mitano na saba.

Katika shitaka la kwanza, Wakili wa Serikali Neema Mwanga alidai mbele ya Hakimu Mkazi Ester Mwakalinga kuwa, Mei 19, mwaka huu saa 1:00 usiku katika eneo la Vingunguti, mshitakiwa alimlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Katika shitaka la pili, Mwanga alidai kuwa Januari 4, mwaka huu katika eneo la Vingunguti kwa Simba, mshitakiwa alimlawiti mtoto wa miaka saba.

Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na kurudishwa rumande kwa kukosa wadhamini, kesi hiyo itatajwa tena Juni 6, mwaka huu.

No comments: