Idara ya polisi nchini Kenya imeanzisha uchunguzi wa mauaji ya wanaharakati wawili wa dini ya Kiislamu ambao hapo awali waliwahi kukabiliwa na mashitaka ya ugaidi. Wanaharakati hao wanadaiwa kulitekwa nyara na watu wasiojulikana yapata siku mbili zilizopita. Wanaharakati hao ambao wote ni wakaazi wa mjini Mombasa ni Ustadh Samir Khan na Sheikh Muhammad Qassim. Inasemekana kuwa wanaharakati hao walipotea katika mazingira ya kutatanisha kabla ya kuuawa na baadaye miili yao kupatikana katika hali ya kustaajabisha. Shirika la Kiislamu la Kutetea Haki za Binadamu nchini Kenya MUHURI limesema kuwa linafuatilia kwa karibu uchunguzi huo ili kujua ukweli wa mambo. Pia viongozi wa Kiislamu nchini humo wamelaani mauaji hayo na kutaka wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Bonyeza hapa kusikiliza ripoti ya mwandishi wa Mombasa, Seifullah Murtadha
No comments:
Post a Comment