Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, April 16, 2012

Sheikh Ponda Issa Ponda: Tanzania kuna udini + Sauti

Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu nchini Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu nchini humo amesema kuwa, suala la udini linaonekana wazi katika siasa za Tanzania ikiwemo pia katika uteuzi wa wajumbe wa Kamati ya Kuratibu Maoni kuhusu Katiba Mpya Tanzania.
Matamshi hayo Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania imekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kuonya kuwa mchakato wa kuandika Katiba Mpya usifanywe kwa kuegemea udini, ukabila, ubinafsi, siasa ama kulenga kuvunja Muungano.
Akizungumza baada ya kuwaapisha wajumbe wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba Mpya, Ikulu, Dar es Salaam, Kikwete alisema, Tanzania hakuna udini wala ukabila.
Tume hiyo itaanza kazi yake ya miezi 18, Mei mosi mwaka huu, kwa kukusanya maoni ya wananchi na kutengeneza rasimu ya katiba, baadaye zikifuata hatua mbili muhimu ambazo ni kuundwa kwa Bunge Maalumu la kuchambua rasimu hiyo, kisha wananchi kupiga kura ya maoni.
Bofya hapa kupata mahojiano aliyofanywa Sheikh Ponda Issa Ponda.

No comments: