Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, April 16, 2012

Baraza la kijeshi Guinea Bissau lafunga redio tatu nchini humo

Baraza la Kijeshi nchini Guienea Bissau limesimamisha shughuli za redio tatu nchini humo.
Habari zinasema kuwa, baraza hilo lilitoa amri ya kufungwa redio tatu zilizokuwa na wasikilizaji wengi ndani ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Sambamba na kufungwa redio hizo tatu, ujumbe wa watu 15 wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika Ecowas uko nchini humo kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro wa nchi hiyo.
Siku ya Ijumaa Ecowas ililaani mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini humo na kutaka kurejeshwa utawala wa katiba haraka iwezekanavyo.

No comments: