Nchi za Magharibi zimekerwa sana na hatua ya Rais Mwai Kibaki wa Kenya ya kuzikumbatia nchi za Mashariki.
Katika ripoti maalumu, toleo la leo la gazeti la Standard la mjini Nairobi limeandika katika toleo la leo kuwa, mashidano kati ya nchi za Magharibi na China kwa lengo la kupata ushawishi katika nchi zinazostawi ni sawa na vita baridi vilivyojiri kati ya Marekani na lililokuwa Shirikisho la Sovieti. Hasira za Wamagharibi kuhusu misimamo huru ya Kenya zilibainika hivi karibuni wakati balozi wa Ufaransa mjini Nairobi Etienne de Poncins aliposema imekuwa vigumu sana kukutana na Rais Kibaki. Katika kumjibu balozi huyo, Ikulu ya Rais Nairobi ilifafanua sababu ya Kenya kuzitenga nchi za Magharibi na kuzikumbatia nchi za Mashariki. Taarifa hiyo ilisema Kibaki ana mtazamo wa kistratijia na anashirikiana na nchi ambazo zinajitahidi kuinua maisha ya Wakenya na watu wa nchi jirani. Ripoti hiyo imemnukulu Waziri wa Mambo ya Nje Kenya Profesa Sam Ongeri akifichua bungeni kuwa, Machi 2010 Rais Kibaki alikataa mwaliko wa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown ambapo alikuwa pia akutane na Malikia Elizabeth. Ongeri amesema hawezi kutoa sababu kamili za Kibaki kukataa mwaliko wa kutembelea Uingereza. Nchi za Magharibi zimeshuhudia kushuka kwa kasi ushawishi wao Kenya huku wakuu wa Nairobi wakizikumbatia nchi kama vile Afrika Kusini, China, India, Korea Kusini na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

1 comment:
Hawa jamaa wanataka nini watuachie na Mashariki yetu......
Post a Comment