Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanapanga mkakati wa kumng'oa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani naye. Duru za karibu na Bunge la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma zinasema kuwa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, sasa yuko katika hatari ya kuondolewa madarakani kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye kufuatia tuhuma nzito za ubadhirifu wa fedha za umma unaodaiwa kuwahusisha mawaziri watano wakiongozwa na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo. Harakati hizo zinaoongozwa na Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma zimeanza kwa hatua ya ukusanyaji saini za Wabunge kwa ajili ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Pinda. Wabunge hao wamewataka mawaziri wanaokabiliwa na kashfa ya ubadhirifu wa fedha kujiuzulu kabla ya Jumatatu la sivyo watawasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment