Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, April 20, 2012

Syria na maombi ya Ban Ki-moon kwa Baraza la Usalama

uku makundi ya upinzani nchini Syria yakiendelea kuvunja makubaliano ya kusimamisha vita nchini humo, Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelitaka Baraza la Usalama la umoja huo liidhinishe kutumwa wasimamiaji 300 wa amani wa kimataifa kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa usitishaji mapigano nchini Syria. Ban ameliandikia barua Baraza la Usalama akisema kuwa, inaonekana wazi kwamba utumiaji nguvu haujasimalizika kikamilifu nchini Syria licha ya kufikiwa makubaliano ya kusimamisha vita na kwamba kuna haja ya kutumwa walinda amani 300 wa kimataifa nchini humo.
Inatarajiwa kuwa wasimamiaji hao watawekwa polepole katika maeneo 10 tofauti ya Syria. Wanadiplomasia wamesema kuwa, azimio linalohusiana na operesheni ya timu hiyo ya Umoja wa Mataifa litakuwa tayari wiki ijayo. Matamshi hayo yamkuja katika hali ambayo jana Alkhamisi ya terhe 19 Aprili, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi nne walishiriki katika mkutano wa mjini Paris Ufaransa ili kujadili suala la Syria. Mkutano huo ulioitishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Alain Marie Juppé, umesusiwa na nchi za Russia na China kwani lengo lake lilikuwa ni kuzidi kuvuruga hali ya mambo nchini Syria. Ni jambo lililo wazi kwamba nchi za Magharibi na vibaraka wao wa Kiarabu hawapendi kuona mgogoro wa Syria unasuluhishwa na ndio maana wanafanya kila njia kuhakikisha kuwa juhudi za Kofi Annan, mpatanishi wa Umoja wa Mataifa na Arab League, zinafeli. Kadiri serikali yenye uungaji mkono mkubwa wa wananchi nchini Syria inavyoonesha nia njema na kukubali mipango mbalimbali ya kimataifa ya kukomesha mgogoro wa nchi hiyo, ndivyo maadui wa taifa hilo wanavyozidi kuweka vizuizi na kuchochea machafuko nchini humo. Siku mbili tu zilizopita, Hillary Clinton, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alisema kuwa Washington itaendelea kuyasaidia kifedha magenge ya kigaidi nchini Syria na kwamba iko tayari kutoa msaada wowote unaotakiwa na magenge hayo ya kigaidi. Uadui huo wa Marekani na vibaraka wake umeongezeka sana hivi sasa baada ya kuonekana mwanga wa kutatuliwa mgogoro wa Syria. Siku chache zilizopita, kundi la kwanza la wasimamiaji wa amani wa kimataifa liliwasili nchini Syria na yote haya yanaonesha ni kiasi gani serikali ya Damascus ilivyo na hamu ya kuona mgogoro wa nchi hiyo unatatuliwa haraka. Hata hivyo hadi hivi sasa maadui wa Syria na makundi yao ya mauaji wameshindwa kuonesha nia ya kweli ya kutatua mgogoro huo, bali wamekuwa wakisisitiza wazi wazi kupewa silaha zaidi makundi ya kigaidi ili yazidi kuchafua hali ya usalama huko Syria. Ni kwa sababu hii ndio maana weledi wa mambo wakasema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kuwashinikiza maadui wa taifa la Syria na magenge yao ya kigaidi yaheshimu juhudi za kimataifa za kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo ambayo inasakamwa kwa sababu tu ya misimamo yake ya kupigania haki na kutokubali kuburuzwa na madola ya kibeberu ya Magharibi.

No comments: