Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, April 12, 2012

UN yahitajia kiasi cha dola bilioni 1 kwa ajili ya matatizo ya wakimbizi

Umoja wa Mataifa umeomba kukusanywa msaada wa kiasi cha dola bilioni 1 kwa ajili ya kutatua matatizo ya wakimbizi katika nchi za Somalia na Sudan.
Masaada huo utahusika kusaida kuboresha maisha, matatizo ya ukosefu wa makazi, kipindupindu na matatizo mengineyo.
Umoja huo wa Mataifa umesema kuwa, unatarajia kuwasaidia wananchi wa Somalia wanaokabiliwa na matatizo chungu nzima yaliyopelekea idadi kubwa ya raia wake kukimbilia katika kambi ya Daabab iliyoko nchini Kenya, sambamba na kutatua matatizo ya raia wa Sudan ambao wanakabiliwa na matatizo ya vita kati ya Sudan na Sudan Kusini.
Aidha ripoti hiyo imesema kuwa, pesa hizo zitatumika katika kukabiliana na baa la njaa lililosababishwa na ukame nchini Somalia na kwamba watu milioni 2.5 wataendelea kuhitajia msaada wa chakula endapo mvua za muda mrefu zitakosa kunyesha nchini humo.

No comments: