Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, April 12, 2012

Kofi Annan akutana na Rais Ahmadinejad, aonya dhidi ya kutumiwa nguvu za kijeshi nchini Syria

Bw. Kofi Annan, mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Arab League kuhusu kadhia ya Syria, jioni ya leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu serikalini hapa jijini Tehran. Kwenye mazungumzo yake na Rais Ahmadinejad, Kofi Annan ameishukuru serikali ya Iran kwa kukubali na kuunga mkono mapendekezo yake ya kutatua mgogoro wa Syria. Katibu Mkuu huyo wa zamani wa UN aidha ametahadharisha kwa mara nyingine tena dhidi ya utumiwaji nguvu za kijeshi kutatua mgogoro wa Syria. Amesema hatua kama hiyo itakuwa na matokeo mabaya ya kujutiwa kwa muda mrefu. Rais Ahmadinejad amesifu juhudi za Annan za kuutafutia ufumbuzi wa amani mgogoro ulioko katika nchi jirani ya Syria. Kabla ya mkutano wake na Rais Ahmadinejad, Kofi Annan alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Ali Akbar Salehi na wakafanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ambapo wanadiplomasia hao wamesisitiza udharura wa kusitishwa mapigano kati ya serikali ya Damascus na magenge ya kigaidi.

No comments: