Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, April 12, 2012

Iran yaendelea kuzikatia nchi za Ulaya mafuta yake

Siku moja baada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutangaza kuwa imesimamisha usambazaji wa mafuta yake kwa Uhispania, Tehran imeamua pia kuikatia mafuta Ujerumani. Wizara inayohusika imesema kuwa hatua hiyo ni katika fremu ya kujibu vikwazo vilivyopitishwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya (EU) dhidi ya Iran mapema mwaka huu.
Mbali na Uingereza, Ufaransa, Ugiriki, Ujerumani na Uhispania ambazo tayari zimeangukiwa na shoka la Iran, Tehran pia inalenga kusitisha usambazaji wa mafuta ghafi Ureno, Uholanzi na Italia. Huku hayo yakijiri, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema itawasilisha mapendekezo mapya kwenye mazungumzo yake na kundi la 5+1 yanayotarajiwa kufanyika mjini Istambul Uturuki baadaye mwezi huu. Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, Saeed Jalili amesema kuwa Iran ina imani kwamba mazungumzo yajayo ya Istambul kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran yatakuwa na manufaa na amezitaka nchi za 5+1 kuingia kwenye mazungumzo hayo bila ya kutoa matamshi ya vitisho na kiburi endapo kweli zina nia ya kutatua sintafahamu iliyopo.
 

No comments: