Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, April 16, 2012

Saeed Jalili: Vikwazo dhidi ya Iran vinaziathiri nchi za Ulaya

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametahadharisha hatua ya Marekani ya kuendeleza vikwazo kwa Tehran na kutilia mkazo kwamba vikwazo hivyo vitakuwa na taathira hasi kwa Ulaya na pia kwa Iran. Jalili amesema hii leo nchi za Ulaya zinagharamika, gharama ambazo nchi hizo hazikustahiki kuzitoa. Amesema muendelezo wa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran unazinyima fursa nchi za Ulaya na kwamba vikwazo hivyo vitakuwa na taathira mbaya kwa uchumi wa nchi hizo. Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo hii ina uwezo mzuri wa kuuza bidhaa zake kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya hususan katika sekta za mafuta na nishati na kwamba nchi hizo hivi sasa zimepoteza fursa katika soko la Iran linalowahudumia watu milioni 70. Amesema iwapo watu hao wote wangeweza kununua bidhaa za Ulaya, uchumi wa Ulaya nao ungenufaika na jambo hilo.

No comments: