Jeshi la Sudan limesema kuwa liko kilomita chache kutoka mji wenye utajiri wa mafuta wa Heglig ambao ulitekwa hivi karibuni na vikosi vamizi vya Sudan Kusini.
Akizungumza Jumamosi jioni, msemaji wa Jeshi la Sudan Sawarmi Khalid Saad amesema lengo ni kuuchukua mji huo , ambao ni milki ya Sudan, bila kusababisha hasara kubwa. Amesema Jeshi la Sudan linalenga kuangamiza jeshi la Sudan Kusini lijulikanalo kama SPLA, na waasi wanaopigana pamoja na jeshi hilo. Waziri wa Habari wa Sudan Abdallah Ali Massar amesema SPLA ikishirikiana na waasi wa JEM kutoka Darfur ilitumia wapiganaji elfu 10 kuukalia kwa mabavu mji wa Heglig Aprili 10.
Jamii ya kimataifa ikiwemo Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Umoja wa Afrika AU zimelaani uvamizi na uliofanywa na Sudan Kusini katika eneo la Heglig huko Kordofan Kusini na zimeitaka Juba kuondoka katika eneo hilo la Sudan haraka iwezekanavyo.

No comments:
Post a Comment