Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, April 16, 2012

Cuf yasema, wananchi ndio watakaoamua hatima ya Muungano

Chama cha Wananchi CUF nchini Tanzania kimesema kuwa, wananchi kupitia mchakato wa wananchi wa Katiba Mpya ndio watakaoamua kuhusu hatima ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kwamba chama hicho kinaamini kuwa tume iliyoundwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete itaweza kufikisha inavyotakiwa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Chama hicho pia kimesema kimeisikia kauli ya Rais Kikwete ya kutoa onyo dhidi ya watu wanaolenga kuvunja muungano lakini pamoja na hayo kimepata faraja kuona kuwa wananchi watapata fursa ya kutoa maoni yao kwa uhuru. Bofya hapa kusikiliza mahojiano tuliyofanya na Bw. Salum Bimani, Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu  wa chama cha CUF.

No comments: