Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, August 3, 2016

Rais wa Sudan Kusini awapiga kalamu nyekundu mawaziri sita wa Machar

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amewapiga kalamu nyekundu mawaziri sita wa upande wa makamu wake wa zamani wa rais yaani Riek Machar.
Akihutubia taifa kupitia televisheni ya serikali, Rais Kiir amesema kuwa, amewafuta kazi mawaziri hao wenye mafungamano na hasimu wake wa kisiasa Riek Machar.
Miongoni mwa mawaziri waliofutwa kazi na Rais Kiir ni pamoja na waziri wa mafuta wa nchi hiyo. Mapigano nchini Sudan Kusini baina ya jeshi la serikali na wapiganaji wa upinzani wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa rais, yaliibuka tangu miaka miwili iliyopita, ambapo zaidi ya watu elfu 10 wameuawa na wengine milioni mbili kuwa wakimbizi. Hata hivyo pande mbili zenye uhasama zilitiliana saini makubaliano ya amani mwaka jana kwa lengo la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa nchini.
 

Pamoja na hayo makubaliano hayo yamekuwa yakikiukwa mara kwa mara, ambapo hivi karibuni yaliibuka mapigano makali mjini Juba, mji mkuu wa nchi hiyo. Kufuatia mapigano hayo, Rais Salva Kiir alimteua Taban Deng Gai kuwa makamu wake wa rais na kumfuta kazi hasimu wake Machar. Hii ni katika hali ambayo weledi wa mambo wameonya juu ya kushadidi machafuko ya kisiasa nchini Sudan Kusini.

No comments: