Soubagleh ameteuliwa kuwa kamanda mpya wa AMISOM katika
mwendelezo wa sera za Umoja wa Mataifa za kupambana na kundi la kigaidi
la ash-Shabab nchini Somalia. Afisa mmoja wa jeshi la Somalia sanjari na
kuthibitisha habari hiyo amesema kuwa, operesheni za kijeshi dhidi ya
wanachama wa kundi hilo zitaendelea kwa ushirikiano mkubwa ya AMISOM.
Osman Nour Soubagleh, Kamanda mpya wa operesheni za AMISOM, Somalia |
Askari wa Umoja wa Afrika nchini Somalia wamepata mafanikio ya
kiwango fulani ikiwa ni pamoja na kurejesha usalama katika baadhi ya
maeneio ya nchi huyo, ingawa wanamgambo wa genge la ash-Shabab wamekuwa
wakifanya hujuma za hapa na pale ndani ya miji tofauti ya nchi hiyo ya
pembe ya Afrika.
Wakati huo huo, Francisco Madeira, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika
nchini Somalia ametangaza kuwa, tangu askari wa umoja huo walipotumwa
nchini Somalia hapo mwaka 2007, wamepata mafanikio makubwa.
Madeira amesema kwa sasa Somalia inaelekea kwenye njia ya amani na utulivu.
No comments:
Post a Comment