Ibrahim al-Awsaj, meya wa mji wa al-Ramadi katikati mwa mkoa wa
al-Anbar, magharibi mwa Iraq, amesema kuwa kufuatia kurejea hali ya
usalama kwa kipindi cha miezi saba iliyopita kwenye maeneo ya mkoa huo,
maelfu ya familia zilizolazimika kuwa wakimbizi kipindi wanachama wa
kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh walipodhibiti maeneo ya mji huo,
sasa zimereja makwao.
Wakimbizi wa Iraq wakirejea makwao baada ya magaidi wa Daesh (ISIS) kufurushwa |
Inafaa kukumbusha kuwa, jeshi la Iraq kwa kushirikiana na harakati za
kujitolea za wananchi, zilianzisha operesheni ya kuukomboa mji wa
al-Ramadi, mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2015.
Wakati huo huo, jeshi la anga nchini Iraq, limeshambulia kwa akali
ngome 20 za wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika
mji wa Mosul wa mkoa wa Nainawa (Nineveh) kaskazini mwa Iraq. Hadi sasa
habari kamili juu ya hasara waliyoipata magaidi hao bado haijawekwa
wazi, ingawa inasadikiwa kuwa idadi kubwa ya wanchama wa genge hilo
wameuawa na zana zao nyingi za kijeshi kuharibiwa.
Raia wa Iraq, wakijaribu kurejea makwao kwa tabu kubwa |
Mashambulizi hayo ni utangulizi wa kuanza kwa operesheni kali za
kuukomboa mji huo kutoka kwa magaidi hao wa Daesh au (ISIS). Mji wa
Mosul ambao ndio ngome kuu ya wanachama wa kundi hilo linaloungwa mkono
na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, ulidhibitiwa mwezi Juni mwaka
2014.
No comments:
Post a Comment