Duru za habari nchini Misri zimedokeza kuwa, kuna uwezekano mkubwa
serikali ya nchi hiyo kutekeleza adhabu ya kifo dhidi ya baadhi ya
viongozi wa harakati iliyopigwa marufuku nchini humo ya Ikhwanul
Muslimin, baada ya likizo za sherehe ya Idil-Fitr.
Gazeti la ash-Sha'ab Misr limewanukuu baadhi ya viongozi wa serikali ya nchi hiyo wakisema kuwa, baadhi ya viongozi wa harakati hiyo wakiwemo Muhammad Badi, kiongozi mkuu wa Ikhwanul Muslimin, na Khayrat ash-Shatir, naibu wa kiongozi mkuu wa harakati hiyo, watanyongwa katika moja ya jela za mji wa Alexandria, kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya Idi.
Viongozi wa
Ikhwanul Muslimin wakiwamo waliotajwa, wanatuhumiwa kwa kuwachochea
wanachama wa harakati hiyo washambulie kituo cha polisi cha al-Arab
katika mji wa Port Said, ambapo makumi ya maafisa wa jeshi la polisi na
askari wa nchi hiyo waliuawa.Gazeti la ash-Sha'ab Misr limewanukuu baadhi ya viongozi wa serikali ya nchi hiyo wakisema kuwa, baadhi ya viongozi wa harakati hiyo wakiwemo Muhammad Badi, kiongozi mkuu wa Ikhwanul Muslimin, na Khayrat ash-Shatir, naibu wa kiongozi mkuu wa harakati hiyo, watanyongwa katika moja ya jela za mji wa Alexandria, kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya Idi.
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali ya Cairo, katika shambulizi hilo, idadi kadhaa ya silaha zilizokuwa katika kituo hicho cha polisi ziliporwa na wavamizi sanjari na kuwaachilia huru mahabusu waliokuwa wakishikiliwa kituoni hapo. Hata hivyo, na licha ya harakati hiyo kupinga tuhuma hizo, bado serikali ya Cairo imeendelea kusisitiza juu ya azma yake ya kutekeleza adhabu ya kifo dhidi ya viongozi hao.
No comments:
Post a Comment