Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, July 18, 2015

Velayati: Njama dhidi ya Uislamu hazitafanikiwa

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu amesema kuwa, njama za wanaoutakia mabaya ulimwengu wa Kiislamu hazitafanikiwa kwa baraka za siku zenye nuru na Eidul Fitr.
Ali Akbar Velayati amesema hayo katika ujumbe wake kwa mnasaba wa Sikukuu ya Eidul Fitr na kusisitiza kuwa, wananchi wa Iran kama ilivyokuwa kwa Waislamu wengine duniani wamefanikiwa kukipitisha kipindi cha mwezi mmoja cha mtihani wa uja ili waweze kupiga hatua kubwa zaidi kwa ajili ya kujenga mustakbali bora katika ulimwengu wa Kiislamu kwa uongozi wa Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei.
Velayati ameashiria katika ujumbe wake huo juu ya kuendelea dhulma na uonevu wa wataka mabaya na njama za maadui katika baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati zikiwemo Yemen, Palestina, Syria, Iraq, Lebanon, Afghanistan, Libya na Pakistan na kubainisha kwamba, makundi yenye kufurutu ada yaliyoko katika ulimwengu wa Kiislamu yameletwa kwa ajili ya kutoa pigo kwa mafundisho ya Kiislamu na kuitambulisha dini hii tukufu kwamba, ni ya utumiaji mabavu.
Dakta Velayati ambaye pia ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kiistratejia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa, kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kuwa ndoto za maadui katika Mashariki ya Kati hazitatimia.

No comments: