William O. Beeman, mhadhiri wa chuo kikuu cha Minnesota nchini Marekani
amesema kuwa, Washington itatengwa endapo kongresi ya nchi hiyo itavunja
makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa hivi karibuni baina ya Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1.
Beeman ameyasema hayo kupitia mahojiano aliyofanyiwa na Shirika la Habari la Mehr ambapo sanjari na kuashiria hotuba ya Rais Barack Obama wa nchi hiyo kuhusiana na makubaliano hayo ambayo yanapingwa na wajumbe wa chama cha Republican, na kusema kuwa, matamshi ya rais huyo ni yenye kugongana.
Aidha
ameashiria propaganda ambazo zimekuwa zikitolewa na kongresi ya Marekani
ya kutaka kupuuzwa makubaliano hayo ya nyuklia na kuongeza kuwa, ikiwa
Warepublicans watafanikiwa kufikia malengo yao hayo, basi ni Marekani
yenyewe ndiyo itakayopata hasara kubwa, kwani wakati huo walimwengu
hawatosubiri tena hadi Washington ijitatulie matatizo yake ya ndani
yasiyo na msingi wowote. Amesema, baada ya hapo walimwengu wao wenyewe
na bila kusubiri idhini ya Marekani wataiondolea vikwazo Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran na kuitenga Washington.Beeman ameyasema hayo kupitia mahojiano aliyofanyiwa na Shirika la Habari la Mehr ambapo sanjari na kuashiria hotuba ya Rais Barack Obama wa nchi hiyo kuhusiana na makubaliano hayo ambayo yanapingwa na wajumbe wa chama cha Republican, na kusema kuwa, matamshi ya rais huyo ni yenye kugongana.
William O. Beeman, mhadhiri wa chuo kikuu cha Minnesota nchini Marekani amesisitiza kuwa, haijawahi kushuhudiwa hata siku moja kwamba Iran ya Kiislamu iliwahi au ilipanga kuunda silaha za maangamizi ya nyuklia na kwamba propaganda zinazotolewa na viongozi wa White House dhidi ya Tehran, hazina ukweli wowote. Amesema kuwa, kustafidi na urutubishaji wa madini ya urani ya nyuklia pekee hakuwezi kupelekea kuzalisha silaha za maangamizi na kuongeza kuwa, zipo nchi 19 duniani zinazorutubisha urani lakini hazimiliki silaha za maangamizi na kwamba Marekani haijawahi kupinga miradi ya nchi hizo kama inavyofanya kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
No comments:
Post a Comment