Akiwa katika kampeni zake za uchaguzi, Rais Pirre Nkurunziza wa Burundi
amedai kwamba ndiye anayelinda na kudhamini amani nchini Burundi. Rais
huyo ambaye anatuhumiwa na wapinzani kwa kuvuruga usalama na amani
nchini amedai katika kampeni zake hizo za uchaguzi kwamba ndiye mtu
pekee anayelinda na kudhamini amani katika nchi hiyo.
Rais Nkurunziza
ambaye yuko chini ya mashinikizo na ukosolewaji mkubwa wa wapinzani na
jamii ya kiraia nchini Burundi kutokana na uamuzi wake wa kugombea kwa
mara ya tatu uchaguzi mkuu wa nchi hiyo jana Ijumaa alipeleka kampeni
zake za uchaguzi katika mikoa miwili ya kaskazini mwa nchi hiyo ambayo
siku chache zilizopita ilishuhudia mapigano kati ya askari wa serikali
na wanamgambo. Akiwa huko Ndora mji ulio umbali wa kilomita 100 kutoka
mji mkuu Bujumbura, Nkurunziza amedai kwamba tokea chama tawala kiingie
madarakani mwaka 2005 hii ni mara ya kwanza kwa Warundi kutozungumzia
suala la ukabila katika uchaguzi mkuu. Uamuzi wa Nkurunziza kutetea kiti
chake cha urais katika uchaguzi mkuu uliopandwa kufanyika tarehe 21 ya
mwezi huu umezua maandamano na malalamiko makubwa ya wananchi wanaosema
kuwa unakinzana wazi na katiba ya nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment