Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, July 18, 2015

Ban alaani shambulizi la kigaidi nchini Nigeria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amelaani shambulizi la kigaidi lililofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria na kupelekea makumi ya watu kuuaa.
Ripoti iliyotolewa leo na Ban Ki-moon imeeleza kuwa, analaani mashambulizi ya siku mbilizi mtawalia katika miji ya Gombe na Damaturu kaskazini mashariki mwa Nigeria ambayo yamepelekea zaidi ya watu 60 kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, ni suala la kusikitisha kuendelea kujiri hujuma za kigaidi nchini Nigeria, hujuma ambazo wahanga wake wakubwa ni raia wasio na hatia.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baadhi ya mashambulizi hayo yalijiri wakati wahanga wake walikuwa wakisali sala ya Iddil-Fitr katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Inaelezwa kuwa, jana Ijumaa mwanamke mmoja aliyeandamana na binti mdogo ambao wote walikuwa wamebeba mada za miripuko, walijiripua katikati ya waumini waliokuwa wakisali sala ya Idi, mjini Damaturu, makao makuu ya jimbo la Yobe, kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambapo zaidi ya watu 50 walipoteza maisha papohapo.
Mbali na kulaani vitendo hivyo, Ban Ki-moon ametangaza kuiunga mkono serikali ya Abuja katika mapambano yake dhidi ya ugaidi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram nchini humo.

No comments: