Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullahil-Udhma
Sayyid Ali Khamenei, amesema kuwa, mikono michafu ya viongozi waovu,
iliifanya kuwa chungu Ramadhani ya mwaka huu ya watu wa eneo la
Mashariki ya Kati.
Kiongozi Muadhamu, ameyasema hayo leo asubuhi katika hotuba aliyoitoa baada ya sala ya Iddil-Fitr mjini Tehran ambapo ameashiria juu ya migogoro ya eneo, na kusema kuwa mabadiliko yaliyojiri katika eneo ndani ya mwezi wa Ramadhani na kabla yake, yalizifanya kuwa mbaya siku za mwezi huo, kwa Waislamu na waumini wa eneo la Mashariki ya Kati.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia ameashiria
kadhia ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1, ambapo mbali na
kuwasifu wahusika wa mazungumzo hayo marefu na mazito, amesisitiza
kuwa, juhudi za timu ya Iran katika mazungumzo hayo, hazipaswi kufumbiwa
macho, bila kujali kuwa matini ya mapendekezo ya makubaliano hayo
yatapasishwa au la. Amefafanua zaidi kuwa, Iran kamwe haitasalimu amri
mbele ya matakwa ya adui kama vile ambavyo haitaruhusu kutiwa doa muundo
wa mfumo unaotawala nchini hapa. Kiongozi Muadhamu pia amesema kuwa,
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kulinda muundo wake wa kiulinzi
na kiusalama, hata kama maadui wataendelea kufanya njama zao katika
uwanja huo. Ameongeza kuwa, taifa la Iran, litaendelea kuwaunga mkono
marafiki zake katika eneo la Mashariki ya Kati kama vile wananchi wa
mataifa ya Yemen, Palestina, Bahrain, Iraq, Syria na Lebanon, sawa sawa
matini ya makubaliano ya nyuklia yatapasishwa au la.Kiongozi Muadhamu, ameyasema hayo leo asubuhi katika hotuba aliyoitoa baada ya sala ya Iddil-Fitr mjini Tehran ambapo ameashiria juu ya migogoro ya eneo, na kusema kuwa mabadiliko yaliyojiri katika eneo ndani ya mwezi wa Ramadhani na kabla yake, yalizifanya kuwa mbaya siku za mwezi huo, kwa Waislamu na waumini wa eneo la Mashariki ya Kati.
Akiashiria tofauti kubwa zilizopo katika siasa za Iran na Marekani katika eneo amesema kuwa, Marekani inaituhumu Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon kwa ugaidi, katika hali ambayo ni Marekani hiyo hiyo ndiyo inayounga mkono utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ambao ndio asili ya ugaidi na unaoua watoto na wanawake, na kuhoji kuwa ni vipi siasa hizo zinaweza kuwekwa kwenye meza ya mazungumzo na Iran? Amesisitiza kuwa, tangu mwanzo wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, marais wote watano waliotawala Marekani licha ya kufanya njama mbalimbali za kuishinikiza Iran isalimu amri mbele ya taifa hilo, walishindwa na kwamba, wengine wamekufa wakiliacha taifa la Iran ya Kiislamu likiwa bado katika mkondo wake huo.
No comments:
Post a Comment