Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu Iran
amesema, kukiwepo umoja baina ya nchi za Waislamu, magaidi wa kundi la
kitakfiri la Daesh (ISIL) wataangamizwa pasina kuwepo haja ya uingiliaji
majeshi wa kigeni katika ardhi za Waislamu. Mohsen Rezaei ameyasema
hayo mjini Tehran wakati alipokutana na balozi wa Jordan nchini Iran
siku ya Jumamosi. Akiashiria namna magaidi wa Daesh walivyomuua kinyama
robani wa Jordan, Rezai amesema vitendo hama hivyo viitaongeza kasi ya
kuangamia kundi hilo la kigaidi.
Afisa huyo mwandamizi nchini Iran
amesema kuuawa kinyama robani wa Jordan mikononi mwa Daesh ni jambo
ambalo liliamsha hisia za Waislamu na waliowengi duniani dhidi ya Daesh.
Kwa upande wake balozi wa Jordan nchini Iran Abdullah Sulaiman Abdullah
Abdulrahman ameishukuru Iran kwa kulaani mauaji ya robani huyo wa nchi
yake. Ameongeza kuwa nchi za eneo hatimaye zitapata ushindi katika
mapambano dhidi ya Daesh katika vita alivyovitaja kuwa vya kijeshi na
kiutamaduni. Jumanne iliyopita magaidi wa Daesh walionyesha mkanda wa
video wakimchoma kwa moto robani Moaz al-Kassasbeh, aliyetekwa nyara
miezi miwili iliyopita na kundi hilo, suala lililozusha hasira za watu
kote duniani. Baada ya kuoneshwa mkanda huo wa mauaji ya kutisha, Jordan
ilitangaza wanachama wawili wa kundi la kitakfiri la al Qaeda waliokuwa
wakizuiliwa katika jela za nchi hiyo. Aidha Jordan imetekelez
oparesheni kadhaa dhidi ya ngome za Daesh nchini Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment