Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, June 14, 2012

Ndege za Marekani zisizo na rubani zaua watu 30 nchini Yemen

Watu 30 wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na ndege za Marekani zisizo na rubani kusini mwa Yemen. Mashambulizi hayo yaliyofanywa hii leo katika eneo la Ghazan katika mkoa wa Shabu huko kusini mwa nchi hiyo, yaliwalenga wanamgambo wanaodhaniwa kuwa na mafungamano na mtandao wa al Qaida.
Inadaiwa kuwa tangu mwaka uliopita wanamgambo wenye mafungamano na mtandao wa al Qaida walikuwa wanalidhibiti eneo kulikofanyika mashambulizi ya ndege hizo za Marekani.
Katika upande mwingine, vikosi vya Yemen vipatavyo 25 elfu vimekuwa vikiendesha oparesheni kubwa za kijeshi zenye lengo la kuwafurusha wanamgambo wenye silaha katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo, oparesheni ambazo zilianza tangu mwezi uliopita wa Mei.

No comments: