Watu
sita wa familia moja akiwamo Kapteni mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi (JWTZ), wamekufa papo hapo baada ya kuteketezwa kwa moto
jijini Dar es Salaam. Janga hilo la moto limetokea jana saa 10:30 alfajiri katika eneo la Kipunguni A, Ukonga Banana, wilayani Ilala. Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema kuwa moto huo ulizuka
ghafla katika nyumba inayomilikiwa na mstaafu huyo wa Jeshi, David Mpira
anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 55 na 60.
Kamanda
Nzuki alisema wajukuu wa marehemu nao wamekufa katika ajali hiyo, ambao
ni Selina Emmanuel (9) mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya
Msingi Minazi Mirefu na Pauline Emmanuel (3), mwanafunzi wa chekechea
katika Shule ya Tumaini iliyopo Kitunda. “Chanzo
cha moto huo bado hakijafahamika, tunaendelea na uchunguzi na
tunashirikiana na Shirika la Umeme (Tanesco) ili kubaini chanzo
kilichosababisha moto huo,” alisema Nzuki. Maiti wamehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na uchunguzi bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment