Taasisi moja ya Uingereza imetangaza kuwa watoto wadogo ni
wahanga wakuu wa kutumiwa vibaya kijinsia wakati wa vita. Kikao cha siku
nne cha kupambana na vitendo vya utumiaji mbaya wa kijinsia vitani
ambacho kilizishirikisha nchi 100, taasisi zisizo za kiserikali na
wataalamu wa kijeshi kimefanyika huko London Uingereza. Mwishoni mwa
kikao hicho, washiriki wametaka kuweko uungaji mkono wa kimataifa ili
kuweza kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote wanaohusika na
jinai hiyo ya kuwatumia vibaya watoto wadogo kijinsia katika maeneo
yanayokumbwa na vita.
Hii ni katika hali ambayo, Taasisi ya Kuwasaidia Watoto imeeleza kuwa
watoto wadogo aghalabu huwa wahanga wakuu wa vitendo hivyo vilivyotajwa
wakati wa vita. George Graham kutoka Taasisi ya Save The Children
ameeleza kuwa, walimwengu hawapaswi kulipuuza suala hilo na kwamba
wanapaswa kufahamu kuwa watoto ndio wahanga wakuu wa utumiaji mbaya wa
kijinsia wakati wa kujiri vita. Mkutano huo wa London wa kupambana na
vitendo vya kuwatumia vibaya kijinsia watoto wadogo katika maeneo ya
vita umemalizika kwa kuchunguza njia mbalimbali za kukomesha unyanyasaji
huo.
No comments:
Post a Comment