Wanajeshi wenye mfungamano na Russia huko Ukraine wameitungua
ndege ya kijeshi huko katika mji wa Luhansk unaopatikana mashariki mwa
Ukraine. Hayo yamethibitishwa na Wizara ya Ulinzi ya Ukraine. Duru za
kijeshi za Ukraine zimeripoti kuwa ndege hiyo ya usafiri aina ya II-76
imetunguliwa leo na vikosi vya kujilinda vyenye mfungamano na Russia
wakati ikikaribia katika uwanja wa ndege wa mji wa Luhansk.
Abiria
wapatao 50 wanasadikiwa kuwa ndani ya ndege hiyo.Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema kuwa wanajeshi kadhaa wa miavuli na mhudumu mmoja wa ndege wamefariki dunia, huku ripoti nyingine zikibainisha kwamba wanajeshi zaidi ya 30 wameuawa katika tukio hilo.
No comments:
Post a Comment