Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran
yaani bunge amesema kuwa Marekani na waitifaki wake katika eneo la
Mashariki ya Kati wanahusika katika jinai zinazofanywa na makundi ya
Kitakfiri huko Iraq. Ali Larijani amesema madola makubwa yanatumia suala
la ugaidi kama wenzo wao mkuu. Amesema kuwa makundi ya Kitakfiri ambayo
yamekuwa yakiulenga ulimwengu wa Kiislamu yamechafua sura ya Waislamu.
Jeshi la Iraq linaendesha mapambano makali dhidi ya wanamgambo wa
Kitakfiri waliosonga mbele katika mji wa Baaquba kaskazini mwa Baghdad
mji mkuu wa Iraq. Itakumbukwa kuwa, kundi la kigaidi la Daesh wiki hii
liliidhibiti miji miwili ya Tikrit na Mosul ambao ni mji wa pili kwa
ukubwa wa Iraq. Naye Waziri Mkuu wa Iraq Noury al Maliki tarehe kumi
mwezi huu alisema kuwa nchi yake inaendesha vita dhidi ya ugaidi na
kusisitiza kuwa Baghdad kamwe haitaruhusu mji wa Mosul na mkoa wa
Nainavah kuwa chini ya mwavuli wa magaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment