Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa imeziomba nchi
jirani na Jamhuri ya Afrika ya Kati kufungua mipaka yao ili kuwawezesha
wakimbizi wa nchi hiyo kufika katika maeneo yenye amani. Adrian Eduardos
msemaji wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa amesema kuwa
taasisi hiyo inaziomba nchi zote jirani na Jamhuri ya Afrika ya Kati
ikiwemo Chad, kufungua mipaka yake na kuwaruhusu kuingia katika nchi
hizo wakimbizi na wale wanaotafuta hifadhi.
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa Unicef pia umetangaza kuwa wakimbizi wengi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati walioko ndani na nje ya mipaka ya nchi hiyo ni watoto wadogo.
No comments:
Post a Comment