Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa
uchaguzi wa Rais wa tarehe 24 mwezi Khordad sawa na tarehe 14 Juni mwaka
jana ulikuwa hapana kubwa ya taifa la Iran kwa wachupaji mipaka wa
kigeni na wale wa ndani. Dakta Rouhani ameongeza kuwa, ujumbe wa tarehe
24 Khordad mwaka jana ulikuwa huu kwamba, taifa la Iran limechagua njia
ya usawa, amani, urafiki, mapatano, kuamiliana na ulimwengu na njia ya
ustawi madhubuti na wa kudumu, na kwamba njia hiyo ni ya kudumu kwa
ajili ya taifa la Iran.
Rais Rouhani ameyasema hayo leo katika kikao na
waandishi wa habari wa ndani na nje katika maadhimisho ya kwanza ya
hamasa ya kisiasa ya Wairani katika uchaguzi wa Rais uliofanyika mwaka
uliopita hapa nchini.
Rais Hassan Rouhani ameleza kuwa wananchi wa Iran waliutangazia
ulimwengu katika uchaguzi huo kuwa, mashinikizo na vikwazo havitaathiri
malengo makuu na matarajio yao. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
amesisitiza kuwa, iwapo lengo kuu la waweka vikwazo lilikuwa ni kutaka
kuwatenganisha wananchi na mfumo wa Kiislamu, wananchi wa Iran
walitangaza katika masanduku ya kupigia kura kuwa Mapinduzi na mfumo wa
Iran ya Kiislamu kamwe haviwezi kutenganishika, na kwamba mashinikizo na
vikwazo haviwezi kuathiri irada na malengo ya taifa kubwa la Iran.
No comments:
Post a Comment