Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa FAO limetaka misaada ya
haraka ipelekwe nchini Somalia kwa shabaha ya kuondoa matatizo ya
chakula yanayowakabili wananchi wa nchi hiyo. Shirika la FAO
limesisitiza juu ya wasiwasi wa kupatikana dola milioni 18 ambazo
zingeweza kutatua mahitajio ya dharura ya chakula nchini Somalia.
Taarifa ya FAO iliyotolewa jana imeeleza kuwa, kutonyesha mvua na hali
ya hewa kuwa mbaya kumechangia kwa kiasi kikubwa nchi hiyo kutumbukia
kwenye matatizo makubwa ya chakula.
Naye Luca Alinovi Afisa wa FAO
katika nchi za Somalia na Kenya amesema kuwa, hali ya machafuko,
upungufu wa mavuno na maghala ya chakula kuwa matupu katika maeneo makuu
ya uzalishaji chakula ya kusini mwa Somalia, vimechangia kuongezeka bei
ya mahindi kwa asilimia 60 hadi 80 katika kipindi cha mwezi wa Aprili
ikilinganishwa na mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment