Mshauri wa mufti nchini Misri amelitaja kundi linalojiita kwa jina la
Dola la Kiislamu la Iraq na Sham kwa kifupi Daesh kuwa ni kundi lenye
fikra potofu na kwamba ni haramu kwa mtu yeyote kujiunga na kundi hilo.
Ibrahim Najmi amesema kuwa, kundi hilo licha ya kuwa na misimamo
isiyokubalika na Uislamu, limewahadaa vijana wengi kwa kauli ya eti Dola
la Kiislamu, katika hali ambayo vitendo vyake vinafanyika kwa lengo la
kuuchafua Uislamu, kuharibu nchi na kumwaga damu za watu. Amesisitiza
kuwa, ni haramu kujiunga na makundi ya aina hiyo.
Ibrahim ameyasema hayo
katika kikao cha waandishi wa habari katika ofisi ya Kiislamu ya
Darul-Fatwa mjini Cairo, Msri. Aidha amesisitiza kwamba, Watu wanapasa
kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na fikra za makundi yenye
kuuchafulia jina a Uislamu mithili ya Daesh na mengineyo ambayo
yanatekeleza vitendo vya ukatili kote duniani. Amemalizia kwa kusema
kwamba, vitendo vya kundi la Daesh yakiwemo mauaji na uharibifu huko
nchini Iraq, Syria na katika nchi nyingine, vinafanyika kwa maslahi ya
maadui wa umma wa Kiislamu hasa kwa kuzingatia kwamba uharibifu na
mauaji hayo yanafanyika katika nchi za Kiislamu kwa lengo la kuwadhuru
Waislamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment