Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameelezea wasiwasi wa hali ya
usalama na amani kusini mwa nchi hiyo.
Roger Meece amesema kuwa, machafuko yaliyotokea katika jimbo tajiri
kwa madini na maliasili la Katanga, ni jambo lenye kutia wasiwasi
mkubwa. Roger Allen Meece amesisitiza kuwa, kuna ulazima wa kukomeshwa
machafuko kwenye jimbo hilo kwa kutumia njia za kisiasa na mazungumzo.
Mjumbe maalumu wa Ban Ki moon ameongeza kuwa, hatua ya kupelekwa
wanajeshi zaidi katika jimbo la Katanga itasababisha machafuko zaidi
katika eneo hilo.
Wakaazi wa maeneo mashariki mwa Kongo wanakosoa vikali utendaji wa
vikosi vya Umoja wa Mataifa vilivyoko katika eneo hilo kwa kushindwa
kufanya juhudi zozote za kuleta amani.
No comments:
Post a Comment