Viongozi wa Marekani wanafikiria mpango wa kupeleka ndege zisizo na rubani huko kaskazini magharibi mwa Afrika.
Viongozi wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani wamesema kuwa, wanachunguza
mahala itakapowekwa kambi ya ndege hizo katika eneo hilo. Hata hivyo
viongozi hao wamebainisha kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwa ndege hizo
kuwekwa nchini Niger, nchi jirani na Mali. Viongozi hao wameeleza kuwa,
iwapo mpango huo utatekelezwa, Washington itatuma wanajeshi wasiopungua
300 kwenye kambi hiyo. Viongozi hao wa Pentagon wamedai kuwa, lengo la
kuwekwa ndege hizo zisizo na rubani ni kukabiliana na makundi ya kigaidi
kama al Qaeda.
Wakati huohuo, jeshi la Ufaransa limetangaza kuwa, waasi wasiopungua
25 wameuawa kwenye mapigano yaliyojiri siku ya Jumapili katika mji wa
Gao kaskazini mwa Mali.
No comments:
Post a Comment