Hali ya usalama visiwani Zanzibar imeendelea kuwa tete baada ya watu
wasiojulikana kuripuwa bomu nje ya msikiti wa Darajani kisiwani Unguja
na kusababisha taharuki kubwa.
Mtu mmoja ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika tukio hilo
lililotokea baada ya mhadhara uliotolewa baada ya Sala ya Ishaa jana
Ijumaa. Mhadhara huo ulihudhuriwa pia na masheikh kutoka mkoani Tanga na
Mombasa Kenya
Polisi visiwani Zanzibar wamewataka wananchi watulie na wasubiri
kauli rasmi kutoka serikalini, huku uchunguzi kuhusu wahusika wa
shambulio hilo ukiwa umeanza mara moja.
No comments:
Post a Comment