Sheikh Tamim bin Hamad |
Amir mpya wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad bin Khalifa Aal Thani amesema
kuwa nchi hiyo inaliunga mkono kundi kuu la upinzani la Syria
linalojiiita "Baraza la Taifa la Syria." Sheikh Tamim amesema katika
mkutano na wawakilishi wa kundi hilo mjini Doha kuwa mgogoro wa Syria
utaendelea kupewa kipaumbele katika ajenda za siasa za nje za Qatar kama
ilivyokuwa hapo awali. George Sabra, Abdulbasit Sida na Mohamed Farouk
wanaodai ni wawakilishi wa wapinzani wa Syria, wamekutana pia na Khalid
bin Mohammad al Attiyah, Waziri Mpya wa Mambo ya Nje wa Qatar.
Baraza
eti la Taifa la Syria litafanya mkutano mjini Istanbul Uturuki hapo
kesho ili kumchagua kiongozi wake huku Burhan Ghalioun, George Sabra na
Louay M. Safi wakiwania nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment