Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, June 14, 2014

Chama tawala Ivory Coast charidhia maamuzi ya ICC

Chama tawala nchini Ivory Coast kimekaribisha uamuzi wa kuhukumiwa rais wa zamani wan chi hiyo Laurent Gbagbo katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC. Msemaji wa chama hicho Joël N'guessan aliwambia wanachama wa chama hicho hapo jana kuwa, chama tawala kinakubaliana na tuhuma zinazomkabili Gbagbo katika mahakama hiyo na kwamba hatua hiyo itasaidia kuleta usalama nchini humo.
Aidha Joël ameunga mkono uamzi wa ICC wa kukubaliana na tuhuma za jinai dhidi ya binaadamu zinazomkabili mtuhumiwa huyo, na kwamba hatua hiyo italeta furaha kwa familia za wahanga wa matukio ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 nchini humo. Siku ya Alkhamis Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilikubali kuakhirisha kesi ya rais wa zamani wa Kodivaa, Laurent Gbagbo hadi Agosti 13 mwaka huu iliyokuwa imepangiwa kuanza Juni 18 lakini mawakili wa Gbagbo wakasema mteja wao hawezi kuhudhuria vikao vya kesi hiyo kutokana na hali yake mbaya ya kiafya kwa sasa.

No comments: