Makumi ya maelfu ya wananchi wa Burkina Faso
wamendamana katika mji mkuu Ouagadougou kupinga kura ya maoni inayoweza
kumruhusu Rais Blaise Compaore kubakia madarakani kwa mara ya 5.
Zephirin Diabre mtaribu wa maandamano hayo amesema kuwa, hawataki
kipindi kisichokuwa na ukomo cha urais kwani Furkina Faso sio nchi
ambayo kiongozi anatawala hadi pale anapokufa.
Maandamano hayo yalikuwa ni jibu kwa maandamano
yaliyofanywa mwezi uliopita na wafuasi wa rais Compaore ambao wanaunga
mkono kura hiyo ya maoni. Compaore amekuwa rais wa Burkina Farso tangu
mwaka 1987 baada ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi, na ni mshirika muhimu
wa Marekani na Ufaransa katika eneo la Magharibi mwa Afrika.
No comments:
Post a Comment