Askari mmoja wa Marekani aliyekuwa akishikiliwa mateka nchini
Afghanistan ameachiliwa huru kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana
mateka na wanamgambo wa Taliban yaliyosimamiwa na serikali ya Qatar.
Serikali ya Marekani imesema kuwa, Bowe Bergdahl ameachiliwa huru
mkabala wa kuachiliwa huru wafuasi watano muhimu wa Taliban waliokuwa
wakishikiliwa katika jela ya Marekani ya Guantanamo Bay.
Askari huyo wa
Marekani mwenye miaka 28 amekuwa akishikiliwa mateka na Taliban tangu
mwaka 2009 na alikabidhiwa jana kwa vikosi vya Marekani karibu na mpaka
wa Afghanistan na Pakistan.
Wakati huo huo wafungwa watano wa Taliban nao pia wameondoka katika
jela ya Guantanamo Bay kuelekea Qatar. Watano hao wote walikuwa maafisa
wa ngazi za juu wa serikali ya Taliban nchini Afghanistan iliyopinduliwa
na Marekani mwaka 2001.
No comments:
Post a Comment