Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, June 1, 2012

Ash Shabab wathibitisha kupoteza mji muhimu wa Afmadow

Kundi la waasi wa ash Shabab nchini Somalia limethibitisha kuwa mji wa kusini wa Afmadow ambao ni moja ya ngome zake kuu zilizosalia umeingia mikononi mwa vikosi vya pamoja vya Umoja wa Afrika na vya serikali ya Mogadishu. Sheikh Abdiaziz Abu Musab, msemaji wa operesheni za kijeshi wa ash Shabab amesema vikosi vya Kenya na serikali ya Somalia vimeingia katika mji wa Afmadow na wala hakuna mapigano yoyote yaliyotokea katika mji huo. Kundi la ash Shabab limepoteza ngome ya Afmadow miezi saba tangu Kenya ilipotuma vikosi vyake nchini Somalia ikiwa ni sehemu ya operesheni za pande tatu dhidi ya kundi hilo ikijumuisha pia operesheni ya vikosi vya Ethiopia katikati ya nchi hiyo na ile ya vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM karibu na mji mkuu Mogadishu. Kukombolewa kwa Afmadow ni hatua kubwa na muhimu ya kuelekea mji wa kusini wa bandari wa Kismayu ambao ndicho kitovu kikuu cha operesheni za kijeshi za kundi la ash Shabab.../

No comments: